< Zaburi 84 >
1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini!
For the leader. On the gittith. Of the Korahites, a psalm. How dearly loved is the place where you live, Lord of hosts!
2 Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai.
How I long and yearn for the courts of the Lord. Now heart and flesh cry for joy to the living God.
3 Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu.
Even the sparrow has found her a home and the swallow a nest, to lay her young, near your altar, Lord of hosts, my king and my God.
4 Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.
Happy those who live in your house, praising you evermore. (Selah)
5 Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
Happy those whose strength is in you, people with pilgrim hearts.
6 Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.
As they pass through the valley of tears, they make it a place of fountains, clothed with the blessings of early rain.
7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni.
From rampart to rampart on they march, till at last God reveals himself in Zion.
8 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
Lord, God of hosts, hear my prayer, attend, O God of Jacob. (Selah)
9 Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
Behold, O God, our defender, and look upon your anointed,
10 Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
for better a single day in your courts than a thousand in my own chambers: better stand at the door of the house of my God than live in the tents of ungodliness,
11 Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.
for the Lord is sun and shield, the Lord gives grace and glory. He withholds no good thing from the life that is blameless.
12 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.
Lord of hosts, happy those whose trust is in you.