< Zaburi 83 >
1 Wimbo. Zaburi ya Asafu. Ee Mungu, usinyamaze kimya, usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.
亚萨的诗歌。 神啊,求你不要静默! 神啊,求你不要闭口,也不要不作声!
2 Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.
因为你的仇敌喧嚷, 恨你的抬起头来。
3 Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.
他们同谋奸诈要害你的百姓, 彼此商议要害你所隐藏的人。
4 Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”
他们说:来吧,我们将他们剪灭, 使他们不再成国! 使以色列的名不再被人记念!
5 Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, wanafanya muungano dhidi yako,
他们同心商议, 彼此结盟,要抵挡你,
6 mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari,
就是住帐棚的以东人和以实玛利人, 摩押和夏甲人,
7 Gebali, Amoni na Amaleki, Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.
迦巴勒、亚扪, 和亚玛力、非利士并泰尔的居民。
8 Hata Ashuru wameungana nao kuwapa nguvu wazao wa Loti.
亚述也与他们连合; 他们作罗得子孙的帮手。 (细拉)
9 Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini hapo kijito cha Kishoni,
求你待他们,如待米甸, 如在基顺河待西西拉和耶宾一样。
10 ambao waliangamia huko Endori na wakawa kama takataka juu ya nchi.
他们在隐·多珥灭亡, 成了地上的粪土。
11 Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, watawala wao kama Zeba na Salmuna,
求你叫他们的首领像俄立和西伊伯, 叫他们的王子都像西巴和撒慕拿。
12 ambao walisema, “Na tumiliki nchi ya malisho ya Mungu.”
他们说:我们要得 神的住处, 作为自己的产业。
13 Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi yapeperushwayo na upepo.
我的 神啊,求你叫他们像旋风的尘土, 像风前的碎秸。
14 Kama vile moto uteketezavyo msitu au mwali wa moto unavyounguza milima,
火怎样焚烧树林, 火焰怎样烧着山岭,
15 wafuatilie kwa tufani yako na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
求你也照样用狂风追赶他们, 用暴雨恐吓他们。
16 Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.
愿你使他们满面羞耻, 好叫他们寻求你—耶和华的名!
17 Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, na waangamie kwa aibu.
愿他们永远羞愧惊惶! 愿他们惭愧灭亡!
18 Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.
使他们知道:惟独你— 名为耶和华的—是全地以上的至高者!