< Zaburi 82 >

1 Zaburi ya Asafu. Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu.
2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu?
Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? (Selah)
3 Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa.
Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara.
4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu.
5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika.
Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka.
6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu.
7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”
8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.

< Zaburi 82 >