< Zaburi 82 >

1 Zaburi ya Asafu. Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: 2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu? 3 Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. 4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. 5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. 6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ 7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” 8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.

< Zaburi 82 >