< Zaburi 81 >

1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu. Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!
למנצח על-הגתית לאסף ב הרנינו לאלהים עוזנו הריעו לאלהי יעקב
2 Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.
שאו-זמרה ותנו-תף כנור נעים עם-נבל
3 Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume wakati wa Mwandamo wa Mwezi, na wakati wa mwezi mpevu, katika siku ya Sikukuu yetu;
תקעו בחדש שופר בכסה ליום חגנו
4 hii ni amri kwa Israeli, agizo la Mungu wa Yakobo.
כי חק לישראל הוא משפט לאלהי יעקב
5 Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu alipotoka dhidi ya Misri, huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa.
עדות ביהוסף שמו-- בצאתו על-ארץ מצרים שפת לא-ידעתי אשמע
6 Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu.
הסירותי מסבל שכמו כפיו מדוד תעברנה
7 Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba.
בצרה קראת ואחלצך אענך בסתר רעם אבחנך על-מי מריבה סלה
8 “Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!
שמע עמי ואעידה בך ישראל אם-תשמע-לי
9 Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; msimsujudie mungu wa kigeni.
לא-יהיה בך אל זר ולא תשתחוה לאל נכר
10 Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza.
אנכי יהוה אלהיך-- המעלך מארץ מצרים הרחב-פיך ואמלאהו
11 “Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii.
ולא-שמע עמי לקולי וישראל לא-אבה לי
12 Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe.
ואשלחהו בשרירות לבם ילכו במועצותיהם
13 “Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, kama Israeli wangalifuata njia zangu,
לו--עמי שמע לי ישראל בדרכי יהלכו
14 ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!
כמעט אויביהם אכניע ועל צריהם אשיב ידי
15 Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele.
משנאי יהוה יכחשו-לו ויהי עתם לעולם
16 Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora, na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”
ויאכילהו מחלב חטה ומצור דבש אשביעך

< Zaburi 81 >