< Zaburi 80 >
1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu. Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, wewe umwongozaye Yosefu kama kundi; wewe uketiye katika kiti cha enzi katikati ya makerubi, angaza
Usikie, Mchungaji wa Israel, wewe uliye muongoza Yusufu kama kundi; wewe uketiye juu ya makerubi, utuangazie!
2 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. Uamshe nguvu zako, uje utuokoe.
Machoni pa Efraimu na Benjamini na Manase, uziinue nguvu zako; njoo na utuokoe.
3 Ee Mungu, uturejeshe, utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa.
Mungu, uturejeshe sisi; uangaze uso wako juu yetu, nasi tutaokolewa.
4 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi dhidi ya maombi ya watu wako?
Yahwe Mungu wa majeshi, mpaka lini utawakasirikia watu wako wanapoomba?
5 Umewalisha kwa mkate wa machozi, umewafanya wanywe machozi bakuli tele.
Umewalisha wa mkate wa machozi na umewapa machozi ili wanywe katika kiasi kikubwa.
6 Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, na adui zetu wanatudhihaki.
Umetufanya kitu kwa ajili ya majirani zetu kubishania, na maadui zetu hucheka kuhusu sisi kati yao.
7 Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa.
Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; nasi tutaokolewa.
8 Ulileta mzabibu kutoka Misri, ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
Wewe ulileta mzabibu kutoka Misri; ukawafukuza mataifa na ukaupanda.
9 Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
Uliisafisha ardhi kwa ajil yake; nao ulipata mzizi na kuijaza nchi.
10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, mierezi ya Mungu kwa matawi yake.
11 Matawi yake yalienea mpaka Baharini, machipukizi yake mpaka kwenye Mto.
Ilieneza matawi yake mbali kama bahari na mashina yake mpaka kwenye Mto Euphrates.
12 Mbona umebomoa kuta zake ili wote wapitao karibu wazichume zabibu zake?
Kwa nini umezibomoa kuta zake hata wapitao karibu huyachuma matunda yake.
13 Nguruwe mwitu wanauharibu na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
Ngurue wa msituni wanauharibu, na wanyama wa kondeni wanaula.
14 Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! Tazama chini kutoka mbinguni na uone! Linda mzabibu huu,
Urudi, Ee Mungu wa majeshi; kutoka mbinguni utazame chini na uuangalie na kuujali huu mzabibu.
15 mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, mwana uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
Huu ni mzizi ambao mkono wako wa kuume umeupanda, mashina ambayo wewe uliyafanya yakue.
16 Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, unapowakemea, watu wako huangamia.
Yamekatwa na kuchomwa; yameangamia kwa sababu ya kukemea kwako.
17 Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume, mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
Mkono wako na uwe juu ya mtu aliye mkono wako wa kuume, kwa mwana wa mtu uliyemfanya imara kwa ajili yako mwenyewe.
18 Ndipo hatutakuacha tena, utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.
Ndipo hatuta kuacha wewe; utuhuishe, nasi tutaliita jina lako.
19 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa.
Yahwe, Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; utuangazie nuru ya uso wako, nasi tutaokolewa.