< Zaburi 72 >

1 Zaburi ya Solomoni. Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako.
Mpe mfalme amri ya haki yako, Mungu, haki yako kwa wana wa mfalme.
2 Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki.
Naye awaamue watu wako kwa haki na maskini wako kwa haki sawa.
3 Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki.
Milima iwazalie watu amani; vilima navyo vizae haki.
4 Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.
Naye awahukumu watu maskini; awaokoe watoto wa wahitaji na kuwavunja vipande vipande wenye kuwatesa.
5 Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.
Na wakuheshimu wewe wakati wa jua, na kwa kipindi cha kudumu kwa mwezi katika vizazi vyote.
6 Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
Naye apate kuja kama mvua juu ya nyasi zilizokatwa, kama manyuyu yanyunyizayo nchi.
7 Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
Mwenye haki na astawi kwa wakati wake, na amani iwepo kwa wingi mpaka mwezi utakapotoweka.
8 Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.
Na awe na mamlaka toka bahari na bahari, na kutoka Mto hadi miisho ya dunia.
9 Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.
Na wote waishio jangwani wainame mbele zake; adui zake na walambe mavumbi.
10 Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.
Wafalme wa Tashishi na visiwa walete kodi; wafalme wa Sheba na Seba watoe zawadi.
11 Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.
Hakika wafalme wote wamwinamie yeye; mataifa yote yamtumikie yeye.
12 Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
Kwa kuwa yeye humsaidia mhitaji na maskini asiye na msaidizi.
13 Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
Yeye huwahurumia maskini na wahitaji, na huokoa maisha ya wahitaji.
14 Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
Huyaokoa maisha yao dhidi ya mateso na vurugu, na damu yao ni ya thamani machoni pake.
15 Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa.
Naye apate kuishi! Na dhahabu za Sheba apewe yeye. Watu wamuombee yeye siku zote; Mungu ambariki daima.
16 Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni.
Kuwepo na nafaka nyingi katika ardhi; juu ya milima kuwe na mawimbi ya mimea. Matunda yake yawe kama Lebanoni; watu wasitawi katika miji kama nyansi za kondeni.
17 Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.
Jina lake lidumu milele; jina lake ilindelee kama vile jua ling'aavyo; watu wabarikiwe katika yeye; mataifa yote wamwite mbarikiwa.
18 Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.
Yahwe Mungu, Mungu wa Israel, atukuzwe, ambaye pekee hufanya mambo ya ajabu.
19 Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake.
Jina lake tukufu litukuzawe milele, nayo nchi yote ijazwe na utukufu wake. Amina, Amina.
20 Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.
Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamemalizika. Kutatu cha tatu

< Zaburi 72 >