< Zaburi 71 >

1 Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe.
בך-יהוה חסיתי אל-אבושה לעולם
2 Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe.
בצדקתך תצילני ותפלטני הטה-אלי אזנך והושיעני
3 Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
היה לי לצור מעון לבוא-- תמיד צוית להושיעני כי-סלעי ומצודתי אתה
4 Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.
אלהי--פלטני מיד רשע מכף מעול וחומץ
5 Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.
כי-אתה תקותי אדני יהוה מבטחי מנעורי
6 Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima.
עליך נסמכתי מבטן--ממעי אמי אתה גוזי בך תהלתי תמיד
7 Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara.
כמופת הייתי לרבים ואתה מחסי-עז
8 Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.
ימלא פי תהלתך כל-היום תפארתך
9 Usinitupe wakati wa uzee, wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.
אל-תשליכני לעת זקנה ככלות כחי אל-תעזבני
10 Kwa maana adui zangu wananisengenya, wale wanaonivizia kuniua wafanya hila.
כי-אמרו אויבי לי ושמרי נפשי נועצו יחדו
11 Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.”
לאמר אלהים עזבו רדפו ותפשוהו כי-אין מציל
12 Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.
אלהים אל-תרחק ממני אלהי לעזרתי חישה (חושה)
13 Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, wale wanaotaka kunidhuru na wafunikwe kwa dharau na fedheha.
יבשו יכלו שטני נפשי יעטו חרפה וכלמה--מבקשי רעתי
14 Lakini mimi, nitatumaini siku zote, nitakusifu zaidi na zaidi.
ואני תמיד איחל והוספתי על-כל-תהלתך
15 Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake.
פי יספר צדקתך--כל-היום תשועתך כי לא ידעתי ספרות
16 Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja na kutangaza matendo yako makuu, nitatangaza haki yako, yako peke yako.
אבוא--בגברות אדני יהוה אזכיר צדקתך לבדך
17 Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu.
אלהים למדתני מנעורי ועד-הנה אגיד נפלאותיך
18 Ee Mungu, usiniache, hata niwapo mzee wa mvi, mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.
וגם עד-זקנה ושיבה-- אלהים אל-תעזבני עד-אגיד זרועך לדור לכל-יבוא גבורתך
19 Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, wewe ambaye umefanya mambo makuu. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?
וצדקתך אלהים עד-מרום אשר-עשית גדלות אלהים מי כמוך
20 Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, utanihuisha tena, kutoka vilindi vya dunia utaniinua tena.
אשר הראיתנו (הראיתני) צרות רבות-- ורעות תשוב תחינו (תחיני) ומתהמות הארץ תשוב תעלני
21 Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena.
תרב גדלתי ותסב תנחמני
22 Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze.
גם-אני אודך בכלי-נבל-- אמתך אלהי אזמרה לך בכנור-- קדוש ישראל
23 Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha ninapokuimbia sifa, mimi, ambaye umenikomboa.
תרננה שפתי כי אזמרה-לך ונפשי אשר פדית
24 Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki mchana kutwa, kwa maana wale waliotaka kunidhuru, wameaibishwa na kufadhaishwa.
גם-לשוני-- כל-היום תהגה צדקתך כי-בשו כי-חפרו מבקשי רעתי

< Zaburi 71 >