< Zaburi 69 >

1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni.
Al maestro del coro. Su «I gigli». Di Davide. Salvami, o Dio: l'acqua mi giunge alla gola.
2 Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha.
Affondo nel fango e non ho sostegno; sono caduto in acque profonde e l'onda mi travolge.
3 Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu.
Sono sfinito dal gridare, riarse sono le mie fauci; i miei occhi si consumano nell'attesa del mio Dio.
4 Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba.
Più numerosi dei capelli del mio capo sono coloro che mi odiano senza ragione. Sono potenti i nemici che mi calunniano: quanto non ho rubato, lo dovrei restituire?
5 Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako.
Dio, tu conosci la mia stoltezza e le mie colpe non ti sono nascoste.
6 Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.
Chi spera in te, a causa mia non sia confuso, Signore, Dio degli eserciti; per me non si vergogni chi ti cerca, Dio d'Israele.
7 Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu.
Per te io sopporto l'insulto e la vergogna mi copre la faccia;
8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.
sono un estraneo per i miei fratelli, un forestiero per i figli di mia madre.
9 Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.
Poiché mi divora lo zelo per la tua casa, ricadono su di me gli oltraggi di chi ti insulta.
10 Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi.
Mi sono estenuato nel digiuno ed è stata per me un'infamia.
11 Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau.
Ho indossato come vestito un sacco e sono diventato il loro scherno.
12 Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi.
Sparlavano di me quanti sedevano alla porta, gli ubriachi mi dileggiavano.
13 Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika.
Ma io innalzo a te la mia preghiera, Signore, nel tempo della benevolenza; per la grandezza della tua bontà, rispondimi, per la fedeltà della tua salvezza, o Dio.
14 Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji.
Salvami dal fango, che io non affondi, liberami dai miei nemici e dalle acque profonde.
15 Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.
Non mi sommergano i flutti delle acque e il vortice non mi travolga, l'abisso non chiuda su di me la sua bocca.
16 Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie.
Rispondimi, Signore, benefica è la tua grazia; volgiti a me nella tua grande tenerezza.
17 Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.
Non nascondere il volto al tuo servo, sono in pericolo: presto, rispondimi.
18 Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu.
Avvicinati a me, riscattami, salvami dai miei nemici.
19 Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua.
Tu conosci la mia infamia, la mia vergogna e il mio disonore; davanti a te sono tutti i miei nemici.
20 Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata.
L'insulto ha spezzato il mio cuore e vengo meno. Ho atteso compassione, ma invano, consolatori, ma non ne ho trovati.
21 Waliweka nyongo katika chakula changu na walinipa siki nilipokuwa na kiu.
Hanno messo nel mio cibo veleno e quando avevo sete mi hanno dato aceto.
22 Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi.
La loro tavola sia per essi un laccio, una insidia i loro banchetti.
23 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.
Si offuschino i loro occhi, non vedano; sfibra per sempre i loro fianchi.
24 Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate.
Riversa su di loro il tuo sdegno, li raggiunga la tua ira ardente.
25 Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.
La loro casa sia desolata, senza abitanti la loro tenda;
26 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.
perché inseguono colui che hai percosso, aggiungono dolore a chi tu hai ferito.
27 Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako.
Imputa loro colpa su colpa e non ottengano la tua giustizia.
28 Wafutwe kutoka kitabu cha uzima na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.
Siano cancellati dal libro dei viventi e tra i giusti non siano iscritti.
29 Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.
Io sono infelice e sofferente; la tua salvezza, Dio, mi ponga al sicuro.
30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
Loderò il nome di Dio con il canto, lo esalterò con azioni di grazie,
31 Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.
che il Signore gradirà più dei tori, più dei giovenchi con corna e unghie.
32 Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!
Vedano gli umili e si rallegrino; si ravvivi il cuore di chi cerca Dio,
33 Bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa.
poiché il Signore ascolta i poveri e non disprezza i suoi che sono prigionieri.
34 Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake,
A lui acclamino i cieli e la terra, i mari e quanto in essi si muove.
35 kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,
Perché Dio salverà Sion, ricostruirà le città di Giuda: vi abiteranno e ne avranno il possesso.
36 watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo.
La stirpe dei suoi servi ne sarà erede, e chi ama il suo nome vi porrà dimora.

< Zaburi 69 >