< Zaburi 62 >

1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake.
למנצח על ידותון מזמור לדוד אך אל אלהים דומיה נפשי ממנו ישועתי׃
2 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.
אך הוא צורי וישועתי משגבי לא אמוט רבה׃
3 Mtamshambulia mtu hata lini? Je, ninyi nyote mtamtupa chini, ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika?
עד אנה תהותתו על איש תרצחו כלכם כקיר נטוי גדר הדחויה׃
4 Walikusudia kikamilifu kumwangusha toka mahali pake pa fahari; wanafurahia uongo. Kwa vinywa vyao hubariki, lakini ndani ya mioyo yao hulaani.
אך משאתו יעצו להדיח ירצו כזב בפיו יברכו ובקרבם יקללו סלה׃
5 Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake.
אך לאלהים דומי נפשי כי ממנו תקותי׃
6 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika.
אך הוא צורי וישועתי משגבי לא אמוט׃
7 Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu.
על אלהים ישעי וכבודי צור עזי מחסי באלהים׃
8 Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, miminieni mioyo yenu kwake, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.
בטחו בו בכל עת עם שפכו לפניו לבבכם אלהים מחסה לנו סלה׃
9 Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu, nao wa ngazi ya juu ni uongo tu; wakipimwa kwenye mizani, si chochote; wote kwa pamoja ni pumzi tu.
אך הבל בני אדם כזב בני איש במאזנים לעלות המה מהבל יחד׃
10 Usitumainie vya udhalimu wala usijivune kwa vitu vya wizi; ingawa utajiri wako utaongezeka, usiviwekee moyo wako.
אל תבטחו בעשק ובגזל אל תהבלו חיל כי ינוב אל תשיתו לב׃
11 Jambo moja Mungu amelisema, mambo mawili nimeyasikia: kwamba, Ee Mungu, wewe una nguvu,
אחת דבר אלהים שתים זו שמעתי כי עז לאלהים׃
12 na kwamba, Ee Bwana, wewe ni mwenye upendo. Hakika utampa kila mtu thawabu kwa kadiri ya alivyotenda.
ולך אדני חסד כי אתה תשלם לאיש כמעשהו׃

< Zaburi 62 >