< Zaburi 57 >
1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite.
“For the leader of the music. To be sung to the tune of “Do not destroy.” A psalm of David, when he fled from Saul in the cave.” Have pity upon me, O God! have pity upon me, For in thee doth my soul seek refuge! Yea, in the shadow of thy wings do I take shelter, Until these calamities be overpast!
2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.
I call upon God the Most High, Upon God, who performeth all things for me;
3 Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.
He will send from heaven, and save me; He will put to shame him that panteth for my life; (Pause) God will send forth his mercy and his truth.
4 Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali.
My life is in the midst of lions; I dwell among them that breathe out fire; Among men whose teeth are spears and arrows, And whose tongue is a sharp sword.
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote.
Exalt thyself, O God! above the heavens, And thy glory above all the earth!
6 Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe.
They have prepared a net for my steps; My soul is bowed down; They have digged a pit before me, But into it they have themselves fallen.
7 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.
My heart is strengthened, O God! my heart is strengthened! I will sing, and give thanks.
8 Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko.
Awake, my soul! awake, psaltery and harp! I will wake with the early dawn.
9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.
I will praise thee, O Lord! among the nations; I will sing to thee among the kingdoms!
10 Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, uaminifu wako unazifikia anga.
For thy mercy reacheth to the heavens, And thy truth to the clouds!
11 Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, utukufu wako na uwe duniani pote.
Exalt thyself, O God! above the heavens, And thy glory above all the earth!