< Zaburi 55 >

1 Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu.
למנצח בנגינת משכיל לדוד ב האזינה אלהים תפלתי ואל-תתעלם מתחנתי
2 Nisikie na unijibu. Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa
הקשיבה לי וענני אריד בשיחי ואהימה
3 kwa sauti ya adui, kwa kukaziwa macho na waovu, kwa sababu wananiletea mateso juu yangu na kunitukana kwa hasira zao.
מקול אויב--מפני עקת רשע כי-ימיטו עלי און ובאף ישטמוני
4 Moyo wangu umejaa uchungu, hofu ya kifo imenishambulia.
לבי יחיל בקרבי ואימות מות נפלו עלי
5 Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha.
יראה ורעד יבא בי ותכסני פלצות
6 Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika.
ואמר--מי-יתן-לי אבר כיונה אעופה ואשכנה
7 Ningalitorokea mbali sana na kukaa jangwani,
הנה ארחיק נדד אלין במדבר סלה
8 ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.”
אחישה מפלט לי-- מרוח סעה מסער
9 Ee Bwana, uwatahayarishe waovu na uwachanganyishie semi zao, maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.
בלע אדני פלג לשונם כי-ראיתי חמס וריב בעיר
10 Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, uovu na dhuluma vimo ndani yake.
יומם ולילה--יסובבה על-חומתיה ואון ועמל בקרבה
11 Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini, vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake.
הוות בקרבה ולא-ימיש מרחבה תך ומרמה
12 Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia, kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, ningejificha asinione.
כי לא-אויב יחרפני ואשא לא-משנאי עלי הגדיל ואסתר ממנו
13 Kumbe ni wewe, mwenzangu, mshiriki na rafiki yangu wa karibu,
ואתה אנוש כערכי אלופי ומידעי
14 ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri, tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.
אשר יחדו נמתיק סוד בבית אלהים נהלך ברגש
15 Kifo na kiwajie adui zangu ghafula, na washuke kuzimu wangali hai, kwa maana uovu upo ndani yao. (Sheol h7585)
ישימות (ישי מות) עלימו--ירדו שאול חיים כי-רעות במגורם בקרבם (Sheol h7585)
16 Lakini ninamwita Mungu, naye Bwana huniokoa.
אני אל-אלהים אקרא ויהוה יושיעני
17 Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti yangu.
ערב ובקר וצהרים אשיחה ואהמה וישמע קולי
18 Huniokoa nikawa salama katika vita vilivyopangwa dhidi yangu, ingawa watu wengi hunipinga.
פדה בשלום נפשי מקרב-לי כי-ברבים היו עמדי
19 Mungu anayemiliki milele, atawasikia na kuwaadhibu, watu ambao hawabadilishi njia zao, wala hawana hofu ya Mungu.
ישמע אל ויענם-- וישב קדם סלה אשר אין חליפות למו ולא יראו אלהים
20 Mwenzangu hushambulia rafiki zake, naye huvunja agano lake.
שלח ידיו בשלמיו חלל בריתו
21 Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
חלקו מחמאת פיו-- וקרב-לבו רכו דבריו משמן והמה פתחות
22 Mtwike Bwana fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
השלך על-יהוה יהבך-- והוא יכלכלך לא-יתן לעולם מוט-- לצדיק
23 Lakini wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi ninakutumaini wewe.
ואתה אלהים תורדם לבאר שחת-- אנשי דמים ומרמה לא-יחצו ימיהם ואני אבטח-בך

< Zaburi 55 >