< Zaburi 54 >

1 Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
西弗人来对扫罗说:“大卫岂不是在我们那里藏身吗?”那时,大卫作这训诲诗,交与伶长。用丝弦的乐器。 神啊,求你以你的名救我, 凭你的大能为我伸冤。
2 Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.
神啊,求你听我的祷告, 留心听我口中的言语。
3 Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.
因为,外人起来攻击我, 强暴人寻索我的命; 他们眼中没有 神。 (细拉)
4 Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.
神是帮助我的,是扶持我命的。
5 Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.
他要报应我仇敌所行的恶; 求你凭你的诚实灭绝他们。
6 Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.
我要把甘心祭献给你。 耶和华啊,我要称赞你的名;这名本为美好。
7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.
他从一切的急难中把我救出来; 我的眼睛也看见了我仇敌遭报。

< Zaburi 54 >