< Zaburi 51 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.
למנצח מזמור לדוד בבוא אליו נתן הנביא כאשר בא אל בת שבע חנני אלהים כחסדך כרב רחמיך מחה פשעי׃
2 Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.
הרבה כבסני מעוני ומחטאתי טהרני׃
3 Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
כי פשעי אני אדע וחטאתי נגדי תמיד׃
4 Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu.
לך לבדך חטאתי והרע בעיניך עשיתי למען תצדק בדברך תזכה בשפטך׃
5 Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
הן בעוון חוללתי ובחטא יחמתני אמי׃
6 Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.
הן אמת חפצת בטחות ובסתם חכמה תודיעני׃
7 Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
תחטאני באזוב ואטהר תכבסני ומשלג אלבין׃
8 Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.
תשמיעני ששון ושמחה תגלנה עצמות דכית׃
9 Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote.
הסתר פניך מחטאי וכל עונתי מחה׃
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
לב טהור ברא לי אלהים ורוח נכון חדש בקרבי׃
11 Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
אל תשליכני מלפניך ורוח קדשך אל תקח ממני׃
12 Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze.
השיבה לי ששון ישעך ורוח נדיבה תסמכני׃
13 Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
אלמדה פשעים דרכיך וחטאים אליך ישובו׃
14 Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.
הצילני מדמים אלהים אלהי תשועתי תרנן לשוני צדקתך׃
15 Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako.
אדני שפתי תפתח ופי יגיד תהלתך׃
16 Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa.
כי לא תחפץ זבח ואתנה עולה לא תרצה׃
17 Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.
זבחי אלהים רוח נשברה לב נשבר ונדכה אלהים לא תבזה׃
18 Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.
היטיבה ברצונך את ציון תבנה חומות ירושלם׃
19 Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, pia mafahali watatolewa madhabahuni mwako.
אז תחפץ זבחי צדק עולה וכליל אז יעלו על מזבחך פרים׃

< Zaburi 51 >