< Zaburi 48 >

1 Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu.
科辣黑後裔的詩歌。 在我們天主的城池中,上主至大,應受到讚頌。
2 Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya Safoni ni Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu.
祂的聖山巍峨高聳,是普世的歡喜,北方中心熙雍聖山,是大王的城邑。
3 Mungu yuko katika ngome zake; amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.
天主居於堡壘的中央,顯自己為穩固的保障。
4 Wakati wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja,
請看,眾王紛紛相聚,他們蜂擁走向前去,
5 walimwona nao wakashangaa, wakakimbia kwa hofu.
他們一見,驚魂喪膽,張惶失措,抱頭鼠竄。
6 Kutetemeka kuliwashika huko, maumivu kama ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa.
他們在那裡惶懼恐怖,苦痛有如臨盆的孕婦;
7 Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki.
好像塔爾史士的船隻,為強烈的東風所襲擊。
8 Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele.
在萬軍上主的城裏,即我們天主的城堡,我們所見正如所聞:天主必使城堡永固。
9 Ee Mungu, hekaluni mwako tunatafakari upendo wako usiokoma.
天主,我們在你的殿裏,沉思默念著你的仁慈。
10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki.
天主,你的名號遠達地極,你受的讚美亦應該如此。你的右手全充滿了正義,
11 Mlima Sayuni unashangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako.
願熙雍山因你的公正而喜樂;猶大女子也要因此歡欣踴躍。
12 Tembeeni katika Sayuni, uzungukeni mji, hesabuni minara yake;
你們環繞熙雍巡遊,你們數點她的城樓,
13 yatafakarini vyema maboma yake, angalieni ngome zake, ili mpate kusimulia habari zake kwa kizazi kijacho.
觀察她的城廓,巡視她的碉堡,是為叫你們向後代子孫陳述:
14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.
天主的確是偉大的天主,也永遠是我們的天主,始終領導我們的天主。

< Zaburi 48 >