< Zaburi 47 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe!
Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi.
2 Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote!
Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote.
3 Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu.
Yeye anawatiisha chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu.
4 Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda.
Yeye huchagua urithi kwa ajili yetu, utukufu wa Yakobo ambaye alimpenda. Serah
5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta.
Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu.
6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa.
Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa.
8 Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi.
9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.
Wakuu wa watu wamekusanyika pamoja kwa watu wa Mungu wa Ibrahimu; kwa kuwa ngao za duniani ni za Mungu; yeye ameinuliwa juu sana.

< Zaburi 47 >