< Zaburi 45 >
1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi. Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.
My heart is gushing a good matter: I speak of the things which I have made touching the king: my tongue is the pen of a ready writer.
2 Wewe ni bora kuliko watu wengine wote na midomo yako imepakwa neema, kwa kuwa Mungu amekubariki milele.
You are fairer than the children of men: grace is poured into your lips: therefore God has blessed you for ever.
3 Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu.
Gird your sword on your thigh, O most mighty, with your glory and your majesty.
4 Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi, kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.
And in your majesty ride prosperously because of truth and meekness and righteousness; and your right hand shall teach you terrible things.
5 Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme, mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako.
Your arrows are sharp in the heart of the king’s enemies; whereby the people fall under you.
6 Ee Mungu, kiti chako cha enzi kitadumu milele na milele, fimbo ya utawala wa haki itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.
Your throne, O God, is for ever and ever: the scepter of your kingdom is a right scepter.
7 Unaipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako, kwa kukupaka mafuta ya furaha.
You love righteousness, and hate wickedness: therefore God, your God, has anointed you with the oil of gladness above your fellows.
8 Mavazi yako yote yana harufu nzuri ya manemane, udi na mdalasini; kutoka kwenye majumba ya kifalme yaliyopambwa kwa pembe za ndovu, sauti za vinanda vya nyuzi zinakufanya ufurahi.
All your garments smell of myrrh, and aloes, and cassia, out of the ivory palaces, whereby they have made you glad.
9 Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa; kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.
Kings’ daughters were among your honorable women: on your right hand did stand the queen in gold of Ophir.
10 Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio: Sahau watu wako na nyumba ya baba yako.
Listen, O daughter, and consider, and incline your ear; forget also your own people, and your father’s house;
11 Mfalme ameshangazwa na uzuri wako; mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako.
So shall the king greatly desire your beauty: for he is your Lord; and worship you him.
12 Binti wa Tiro atakuletea zawadi, watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako.
And the daughter of Tyre shall be there with a gift; even the rich among the people shall entreat your favor.
13 Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake; vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.
The king’s daughter is all glorious within: her clothing is of worked gold.
14 Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, mabikira wenzake wanamfuata na wanaletwa kwako.
She shall be brought to the king in raiment of needlework: the virgins her companions that follow her shall be brought to you.
15 Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, na kuingia katika jumba la mfalme.
With gladness and rejoicing shall they be brought: they shall enter into the king’s palace.
16 Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, mtawafanya wakuu katika nchi yote.
Instead of your fathers shall be your children, whom you may make princes in all the earth.
17 Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.
I will make your name to be remembered in all generations: therefore shall the people praise you for ever and ever.