< Zaburi 41 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida.
達味詩歌,交與樂官。 眷顧貧窮人的人,真是有福,患難時日,他必蒙上主救助。
2 Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.
上主必保護他,賜他生存,在世上蒙福,決不將他交給他的仇敵而任敵所欲。
3 Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake.
他呻吟床榻,上主給他支援,他患病時,必使他轉危為安。
4 Nilisema, “Ee Bwana nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”
我曾哀求你:上主,求你憐憫我」,求你治癒我,因為我得罪了你。
5 Adui zangu wanasema kwa hila, “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”
我的仇敵反而惡言辱罵我說:「他何時死,他的名字幾時泯滅?
6 Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.
前來訪我的人,只以虛言相待,其實是心懷惡意,出去便說出來。
7 Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, hao huniwazia mabaya sana, wakisema,
恨我的人,個個竊竊私議,咒我遭殃生疾:
8 “Ugonjwa mbaya sana umempata, kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”
願他身患惡疾! 願他一病不起!
9 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake.
連我素來信賴的知心友好,吃過我飯的人,也舉腳踢我。
10 Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.
上主,求你可憐我,使我病除,為使我能對他們加以復仇。
11 Najua kwamba wapendezwa nami, kwa kuwa adui yangu hanishindi.
我以此作為你真愛我的記號:就是不讓我的敵人向我誇耀;
12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele.
你時常保持我無災無難,使我永遠站在你的面前。
13 Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele.
願上主,以色列天主,受讚頌,自永遠直到永遠,阿們,阿們

< Zaburi 41 >