< Zaburi 36 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana. Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
למנצח לעבד-יהוה לדוד ב נאם-פשע לרשע בקרב לבי אין-פחד אלהים לנגד עיניו
2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.
כי-החליק אליו בעיניו למצא עונו לשנא
3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.
דברי-פיו און ומרמה חדל להשכיל להיטיב
4 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya.
און יחשב--על-משכבו יתיצב על-דרך לא-טוב רע לא ימאס
5 Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga.
יהוה בהשמים חסדך אמונתך עד-שחקים
6 Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama.
צדקתך כהררי-אל--משפטיך תהום רבה אדם ובהמה תושיע יהוה
7 Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.
מה-יקר חסדך אלהים ובני אדם--בצל כנפיך יחסיון
8 Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.
ירוין מדשן ביתך ונחל עדניך תשקם
9 Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru.
כי-עמך מקור חיים באורך נראה-אור
10 Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.
משך חסדך לידעיך וצדקתך לישרי-לב
11 Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, wala mkono wa mwovu usinifukuze.
אל-תבואני רגל גאוה ויד-רשעים אל-תנדני
12 Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka!
שם נפלו פעלי און דחו ולא-יכלו קום

< Zaburi 36 >