< Zaburi 35 >

1 Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami, upigane na hao wanaopigana nami.
לדוד ריבה יהוה את יריבי לחם את לחמי׃
2 Chukua ngao na kigao. Inuka unisaidie.
החזק מגן וצנה וקומה בעזרתי׃
3 Inua mkuki wako na fumo lako dhidi ya hao wanaonifuatia. Iambie nafsi yangu, “Mimi ni wokovu wako.”
והרק חנית וסגר לקראת רדפי אמר לנפשי ישעתך אני׃
4 Wafedheheshwe na waaibishwe wale wanaotafuta uhai wangu. Wanaofanya shauri kuniangamiza warudishwe nyuma kwa hofu.
יבשו ויכלמו מבקשי נפשי יסגו אחור ויחפרו חשבי רעתי׃
5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo, malaika wa Bwana akiwafukuza.
יהיו כמץ לפני רוח ומלאך יהוה דוחה׃
6 Njia yao na iwe giza na ya utelezi, malaika wa Bwana akiwafuatilia.
יהי דרכם חשך וחלקלקות ומלאך יהוה רדפם׃
7 Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu, na bila sababu wamenichimbia shimo,
כי חנם טמנו לי שחת רשתם חנם חפרו לנפשי׃
8 maafa na yawapate ghafula: wavu walionifichia na uwatege wenyewe, na waanguke katika shimo hilo, kwa maangamizo yao.
תבואהו שואה לא ידע ורשתו אשר טמן תלכדו בשואה יפל בה׃
9 Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana na kuufurahia wokovu wake.
ונפשי תגיל ביהוה תשיש בישועתו׃
10 Nitapaza sauti yangu nikisema, “Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana? Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao, maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!”
כל עצמותי תאמרנה יהוה מי כמוך מציל עני מחזק ממנו ועני ואביון מגזלו׃
11 Mashahidi wakatili wanainuka, wananiuliza mambo nisiyoyajua.
יקומון עדי חמס אשר לא ידעתי ישאלוני׃
12 Wananilipa baya kwa jema na kuiacha nafsi yangu ukiwa.
ישלמוני רעה תחת טובה שכול לנפשי׃
13 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia na nikajinyenyekesha kwa kufunga. Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,
ואני בחלותם לבושי שק עניתי בצום נפשי ותפלתי על חיקי תשוב׃
14 niliendelea kuomboleza kama vile wao ni rafiki au ndugu. Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni kama ninayemwombolezea mama yangu.
כרע כאח לי התהלכתי כאבל אם קדר שחותי׃
15 Lakini nilipojikwaa, walikusanyika kwa shangwe; washambuliaji walijikusanya dhidi yangu bila mimi kujua. Walinisingizia pasipo kukoma.
ובצלעי שמחו ונאספו נאספו עלי נכים ולא ידעתי קרעו ולא דמו׃
16 Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki, wamenisagia meno.
בחנפי לעגי מעוג חרק עלי שנימו׃
17 Ee Bwana, utatazama mpaka lini? Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, uhai wangu wa thamani kutokana na simba hawa.
אדני כמה תראה השיבה נפשי משאיהם מכפירים יחידתי׃
18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, nitakusifu katikati ya watu wengi.
אודך בקהל רב בעם עצום אהללך׃
19 Usiwaache wale wanaonisimanga, wale ambao ni adui zangu bila sababu; usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu wakonyeze jicho kwa hila.
אל ישמחו לי איבי שקר שנאי חנם יקרצו עין׃
20 Hawazungumzi kwa amani, bali wanatunga mashtaka ya uongo dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi.
כי לא שלום ידברו ועל רגעי ארץ דברי מרמות יחשבון׃
21 Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha! Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.”
וירחיבו עלי פיהם אמרו האח האח ראתה עינינו׃
22 Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya. Usiwe mbali nami, Ee Bwana.
ראיתה יהוה אל תחרש אדני אל תרחק ממני׃
23 Amka, inuka unitetee! Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu.
העירה והקיצה למשפטי אלהי ואדני לריבי׃
24 Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu, sawasawa na haki yako; usiwaache wakusimange.
שפטני כצדקך יהוה אלהי ואל ישמחו לי׃
25 Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” Au waseme, “Tumemmeza.”
אל יאמרו בלבם האח נפשנו אל יאמרו בלענוהו׃
26 Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau.
יבשו ויחפרו יחדו שמחי רעתי ילבשו בשת וכלמה המגדילים עלי׃
27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”
ירנו וישמחו חפצי צדקי ויאמרו תמיד יגדל יהוה החפץ שלום עבדו׃
28 Ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa.
ולשוני תהגה צדקך כל היום תהלתך׃

< Zaburi 35 >