< Zaburi 34 >

1 Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
לדוד בשנותו את טעמו לפני אבימלך ויגרשהו וילך אברכה את יהוה בכל עת תמיד תהלתו בפי׃
2 Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.
ביהוה תתהלל נפשי ישמעו ענוים וישמחו׃
3 Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
גדלו ליהוה אתי ונרוממה שמו יחדו׃
4 Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
דרשתי את יהוה וענני ומכל מגורותי הצילני׃
5 Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
הביטו אליו ונהרו ופניהם אל יחפרו׃
6 Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.
זה עני קרא ויהוה שמע ומכל צרותיו הושיעו׃
7 Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.
חנה מלאך יהוה סביב ליראיו ויחלצם׃
8 Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.
טעמו וראו כי טוב יהוה אשרי הגבר יחסה בו׃
9 Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote.
יראו את יהוה קדשיו כי אין מחסור ליראיו׃
10 Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
כפירים רשו ורעבו ודרשי יהוה לא יחסרו כל טוב׃
11 Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana.
לכו בנים שמעו לי יראת יהוה אלמדכם׃
12 Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema,
מי האיש החפץ חיים אהב ימים לראות טוב׃
13 basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.
נצר לשונך מרע ושפתיך מדבר מרמה׃
14 Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.
סור מרע ועשה טוב בקש שלום ורדפהו׃
15 Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
עיני יהוה אל צדיקים ואזניו אל שועתם׃
16 Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
פני יהוה בעשי רע להכרית מארץ זכרם׃
17 Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.
צעקו ויהוה שמע ומכל צרותם הצילם׃
18 Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.
קרוב יהוה לנשברי לב ואת דכאי רוח יושיע׃
19 Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
רבות רעות צדיק ומכלם יצילנו יהוה׃
20 huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.
שמר כל עצמותיו אחת מהנה לא נשברה׃
21 Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa.
תמותת רשע רעה ושנאי צדיק יאשמו׃
22 Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe.
פודה יהוה נפש עבדיו ולא יאשמו כל החסים בו׃

< Zaburi 34 >