< Zaburi 31 >
1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe.
For the leader. A psalm of David. In you, O Lord, I take refuge; let me never be put to shame. Rescue me in your faithfulness;
2 Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka; uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa.
incline to me your ear. Deliver me speedily. Be to me a rock of defence, a fortified house, to save me.
3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.
For my rock and my fortress are you; lead me and guide me so your name will be honored.
4 Uniepushe na mtego niliotegewa, maana wewe ndiwe kimbilio langu.
Draw me out of the net they have hid for me, for you yourself are my refuge.
5 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli.
Into your hand I commend my spirit: you ransom me, Lord, faithful God.
6 Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili; mimi ninamtumaini Bwana.
I hate those devoted to worthless idols; I trust in the Lord.
7 Nitafurahia na kushangilia upendo wako, kwa kuwa uliona mateso yangu na ulijua maumivu ya nafsi yangu.
I will rejoice and be glad in your love, because you have looked on my misery, and cared for me in my distress.
8 Hukunikabidhi kwa adui yangu bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi.
You have not given me into the enemy’s hand, you have set my feet in a spacious place.
9 Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; macho yangu yanafifia kwa huzuni, nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.
Be gracious to me, Lord, for I am distressed; my eye is wasted away with sorrow.
10 Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.
For my life is consumed with grief, and my years with sighing. My strength is broken with misery, my bones waste away.
11 Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na jirani zangu, hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, wale wanionao barabarani hunikimbia.
The scorn of all my foes, the butt of my neighbors am I, a terror to my acquaintance. At the sight of me in the street people turn quickly away.
12 Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa, nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika.
I am clean forgotten like the dead, am become like a ruined vessel.
13 Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua.
I hear the whispers of many – terror on every side – scheming together against me, plotting to take my life.
14 Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana; nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”
But my trust is in you, Lord. “You are my God,” I say;
15 Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao.
my times are in your hand, save me from the hand of the foes who pursue me.
16 Mwangazie mtumishi wako uso wako, uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.
Make your face to shine on your servant, save me in your love.
17 Usiniache niaibike, Ee Bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu. (Sheol )
Put me not, O Lord, to shame, for I have called upon you. Let the wicked be put to shame silent in Sheol. (Sheol )
18 Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau wao husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki.
Strike the false lips dumb, that speak proudly against the righteous with haughtiness and contempt.
19 Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako, uliowawekea akiba wakuchao, ambao huwapa wale wakukimbiliao machoni pa watu.
How great is the goodness you have treasured for those who fear you, and wrought for those who take refuge in you, in plain sight of all!
20 Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako kutokana na hila za wanadamu; katika makao yako huwaweka salama kutokana na ndimi za mashtaka.
In your sheltering wings you hide them from plottings of people, you keep them safe in a bower from the chiding of tongues.
21 Atukuzwe Bwana, kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu nilipokuwa katika mji uliozingirwa.
Blest be the Lord for the wonderful love he has shown me in time of distress.
22 Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie.
For I had said in panic, “I am driven clean out of your sight.” But you heard my plea, when I cried to you for help.
23 Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote! Bwana huwahifadhi waaminifu, lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.
Love the Lord, all you faithful; the Lord protects the loyal, but repays the haughty in full.
24 Kuweni hodari na mjipe moyo, ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.
Let your hearts be courageous and strong, all you who wait on the Lord.