< Zaburi 29 >
1 Zaburi ya Daudi. Mpeni Bwana, enyi mashujaa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.
Mpeni sifa Yahwe, enyi wana wa Mungu! Mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu.
2 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
Mpeni Yahwe utukufu ambao jina lake linastahili. Mpigieni magoti Yahwe katika mapambo ya utakatifu.
3 Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
Sauti ya Yahwe imesikika zaidi ya maji; Mungu wa radi ya utukufu, radi yaYahwe i juu ya maji mengi.
4 Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu.
Sauti ya Yahwe ina nguvu; sauti ya Yahwe ni kuu.
5 Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni.
Sauti ya Yahwe huivunja mierezi; Yahwe huivunja vipande vipande mierezi ya Lebanon.
6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni urukaruke kama mwana nyati.
Yeye huifanya Lebanoni kuruka kama ndama wa ng'ombe na Sirioni kama mwana wa nyati.
7 Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi.
Sauti ya Yahwe hutoa miale ya moto.
8 Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
Sauti ya Yahwe hutetemesha Jangwa; Yahwe hutetemesha jangwa la Kadeshi.
9 Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!”
Sauti ya Yahwe huufanya miti mikubwa kutikisika na huipukutisha misitu. Kila mmoja katika hekalu lake husema, “Utukufu!”
10 Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.
Yahwe hukaa kama mfalme juu ya mafuriko; Yahwe hukaa kama mfalme milele.
11 Bwana huwapa watu wake nguvu; Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.
Yahwe huwatia nguvu watu wake; Yahwe huwa bariki watu wake na amani.