< Zaburi 27 >

1 Zaburi ya Daudi. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani?
לדוד יהוה אורי וישעי ממי אירא יהוה מעוז חיי ממי אפחד׃
2 Waovu watakaposogea dhidi yangu ili wanile nyama yangu, adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia, watajikwaa na kuanguka.
בקרב עלי מרעים לאכל את בשרי צרי ואיבי לי המה כשלו ונפלו׃
3 Hata jeshi linizunguke pande zote, moyo wangu hautaogopa; hata vita vitokee dhidi yangu, hata hapo nitakuwa na ujasiri.
אם תחנה עלי מחנה לא יירא לבי אם תקום עלי מלחמה בזאת אני בוטח׃
4 Jambo moja ninamwomba Bwana, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kumtafuta hekaluni mwake.
אחת שאלתי מאת יהוה אותה אבקש שבתי בבית יהוה כל ימי חיי לחזות בנעם יהוה ולבקר בהיכלו׃
5 Kwa kuwa siku ya shida, atanihifadhi salama katika maskani yake, atanificha uvulini mwa hema yake na kuniweka juu kwenye mwamba.
כי יצפנני בסכה ביום רעה יסתרני בסתר אהלו בצור ירוממני׃
6 Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Bwana na kumsifu.
ועתה ירום ראשי על איבי סביבותי ואזבחה באהלו זבחי תרועה אשירה ואזמרה ליהוה׃
7 Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, unihurumie na unijibu.
שמע יהוה קולי אקרא וחנני וענני׃
8 Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”
לך אמר לבי בקשו פני את פניך יהוה אבקש׃
9 Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu.
אל תסתר פניך ממני אל תט באף עבדך עזרתי היית אל תטשני ואל תעזבני אלהי ישעי׃
10 Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, Bwana atanipokea.
כי אבי ואמי עזבוני ויהוה יאספני׃
11 Nifundishe njia yako, Ee Bwana, niongoze katika njia iliyonyooka kwa sababu ya watesi wangu.
הורני יהוה דרכך ונחני בארח מישור למען שוררי׃
12 Usiniachilie kwa nia za adui zangu, kwa maana mashahidi wa uongo wameinuka dhidi yangu, wakipumua ujeuri.
אל תתנני בנפש צרי כי קמו בי עדי שקר ויפח חמס׃
13 Nami bado nina tumaini hili: nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
לולא האמנתי לראות בטוב יהוה בארץ חיים׃
14 Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.
קוה אל יהוה חזק ויאמץ לבך וקוה אל יהוה׃

< Zaburi 27 >