< Zaburi 25 >

1 Zaburi ya Daudi. Kwako wewe, Ee Bwana, nainua nafsi yangu,
Of David. To You, O LORD, I lift up my soul;
2 ni wewe ninayekutumainia, Ee Mungu wangu. Usiniache niaibike, wala usiache adui zangu wakanishinda.
in You, my God, I trust. Do not let me be put to shame; do not let my enemies exult over me.
3 Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu.
Surely none who wait for You will be put to shame; but those who are faithless without cause will be disgraced.
4 Nionyeshe njia zako, Ee Bwana, nifundishe mapito yako,
Show me Your ways, O LORD; teach me Your paths.
5 niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.
Guide me in Your truth and teach me, for You are the God of my salvation; all day long I wait for You.
6 Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo, kwa maana zimekuwepo tangu zamani.
Remember, O LORD, Your compassion and loving devotion, for they are from age to age.
7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala njia zangu za uasi, sawasawa na upendo wako unikumbuke, kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana.
Remember not the sins of my youth, nor my rebellious acts; remember me according to Your loving devotion, because of Your goodness, O LORD.
8 Bwana ni mwema na mwenye adili, kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.
Good and upright is the LORD; therefore He shows sinners the way.
9 Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake.
He guides the humble in what is right and teaches them His way.
10 Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.
All the LORD’s ways are loving and faithful to those who keep His covenant and His decrees.
11 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.
For the sake of Your name, O LORD, forgive my iniquity, for it is great.
12 Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana? Atamfundisha katika njia atakayoichagua kwa ajili yake.
Who is the man who fears the LORD? He will instruct him in the path chosen for him.
13 Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi.
His soul will dwell in prosperity, and his descendants will inherit the land.
14 Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake.
The LORD confides in those who fear Him, and reveals His covenant to them.
15 Macho yangu humwelekea Bwana daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego.
My eyes are always on the LORD, for He will free my feet from the mesh.
16 Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka.
Turn to me and be gracious, for I am lonely and afflicted.
17 Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu.
The troubles of my heart increase; free me from my distress.
18 Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote.
Consider my affliction and trouble, and take away all my sins.
19 Tazama adui zangu walivyo wengi, pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!
Consider my enemies, for they are many, and they hate me with vicious hatred.
20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe.
Guard my soul and deliver me; let me not be put to shame, for I take refuge in You.
21 Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako.
May integrity and uprightness preserve me, because I wait for You.
22 Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote!
Redeem Israel, O God, from all its distress.

< Zaburi 25 >