< Zaburi 23 >

1 Zaburi ya Daudi. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. 2 Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, 3 hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4 Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji. 5 Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika. 6 Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

< Zaburi 23 >