< Zaburi 2 >
1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?
Kwa nini mataifa wanafanya dhoruba, kwa nini watu wanafanya njama ambazo zitafeli?
2 Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
Wafalme wa nchi kwa pamoja hushikilia misimamo yao na watawala kwa pamoja hufanya njama kinyume na Yahwe na kinyume na Masihi, wakisema,
3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
“Ngoja tuzikate pingu walizo tufingia sisi na kuzitupa pingu zao.”
4 Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
Yeye aketie katika mbingu atacheka kwa dharau mbele yao; Bwana atawadhihaki wao.
5 Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
Kisha ataongea nao katika hasira yake na kuwaogofya kwa gadhabu yake, akisema,
6 “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
“Mimi mwenyewe nilimpaka mafuta mfalme wa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
7 Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa.
Nami nitatangaza amri ya Yahwe. Yeye aliniambia, “wewe ni mwanangu! Leo hii nimekuwa baba yako.
8 Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako.
Uniombe, nami nitakupa wewe taifa kwa ajili ya urithi na mikoa ya nchi iliyo bora kwa ajili ya umiliki wako.
9 Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
Wewe utawavunja wao kwa fimbo ya chuma; kama vile mtungi wa mfinyanzi, wewe utawavunja wao vipande vipande.”
10 Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
Hivyo sasa, ninyi wafalme; mchukue tahadhari; mjirekebishe.
11 Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.
Mwabuduni Yahwe kwa hofu na mfurahi mkitetemeka.
12 Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.
Mumbusu mwana vinginevyo atawakasirikia, na mtakufa pale pale hasira yake ikiwaka. Ni jinsi gani wamebarikiwa wale wote watafutao usalama ndani yake.