< Zaburi 2 >

1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?
Why do the nations rage, and the peoples plot in vain?
2 Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
The kings of the earth take a stand, and the rulers take counsel together, against the LORD, and against his Anointed:
3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
"Let's tear off their shackles, and throw off their ropes from us."
4 Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
The one who sits in the heavens laughs. The LORD scoffs at them.
5 Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
Then he will speak to them in his anger, and terrify them in his wrath:
6 “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
"But I myself have installed my king on Zion, my holy mountain."
7 Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa.
I will tell of the decree. The LORD said to me, "You are my son. Today I have become your father.
8 Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako.
Ask of me, and I will give the nations as your inheritance, and the farthest parts of the earth for your possession.
9 Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
You shall rule them with an iron scepter. You shall dash them in pieces like a potter's vessel."
10 Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
Now therefore, you kings, be wise; receive correction, you judges of the earth.
11 Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.
Serve the LORD with fear, and rejoice with trembling.
12 Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.
Do homage in purity, lest he be angry, and you perish in the way, when his anger is suddenly kindled. Blessed are all those who take refuge in him.

< Zaburi 2 >