< Zaburi 17 >

1 Sala ya Daudi. Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.
תפלה לדוד שמעה יהוה צדק הקשיבה רנתי האזינה תפלתי בלא שפתי מרמה׃
2 Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki.
מלפניך משפטי יצא עיניך תחזינה מישרים׃
3 Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi.
בחנת לבי פקדת לילה צרפתני בל תמצא זמתי בל יעבר פי׃
4 Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
לפעלות אדם בדבר שפתיך אני שמרתי ארחות פריץ׃
5 Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.
תמך אשרי במעגלותיך בל נמוטו פעמי׃
6 Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu.
אני קראתיך כי תענני אל הט אזנך לי שמע אמרתי׃
7 Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.
הפלה חסדיך מושיע חוסים ממתקוממים בימינך׃
8 Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako
שמרני כאישון בת עין בצל כנפיך תסתירני׃
9 kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.
מפני רשעים זו שדוני איבי בנפש יקיפו עלי׃
10 Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno.
חלבמו סגרו פימו דברו בגאות׃
11 Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini.
אשרינו עתה סבבוני עיניהם ישיתו לנטות בארץ׃
12 Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.
דמינו כאריה יכסוף לטרוף וככפיר ישב במסתרים׃
13 Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.
קומה יהוה קדמה פניו הכריעהו פלטה נפשי מרשע חרבך׃
14 Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.
ממתים ידך יהוה ממתים מחלד חלקם בחיים וצפינך תמלא בטנם ישבעו בנים והניחו יתרם לעולליהם׃
15 Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.
אני בצדק אחזה פניך אשבעה בהקיץ תמונתך׃

< Zaburi 17 >