< Zaburi 150 >
1 Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.
Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze,
Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi.
4 msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi.
5 msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana.
6 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!
Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe.