< Zaburi 150 >

1 Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze, 4 msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, 5 msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!

< Zaburi 150 >