< Zaburi 15 >
1 Zaburi ya Daudi. Bwana, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu?
Zaburi ya Daudi. Yahwe, ni nani atabaki hemani mwako? Ni nani atakaye ishi kwenye mlima wako mtakatifu?
2 Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,
Yeyote anaye tembea bila lawama, yeye hufanya kilicho haki na huongea ukweli kutoka moyoni mwake.
3 na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake,
Yeye huwa hakashfu kwa ulimi wake, hawadhuru wengine, na hamtusi jirani yake.
4 ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia.
Mtu asiye na maana hudharauliwa machoni pake, bali yeye huwaheshimu wale wanao mhofu Yahwe. Yeye huapa kwa hasara yake mwenyewe na habadilishi ahadi yake.
5 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.
Yeye habadilishi nia yake aazimapo fedha. Yeye hachukui rushwa ili kumshuhudia kinyume asiye na hatia. Yeye afanyanyaye mbambo haya hatatikisika kamwe.