< Zaburi 147 >

1 Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!
הללו יה כי טוב זמרה אלהינו כי נעים נאוה תהלה׃
2 Bwana hujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni.
בונה ירושלם יהוה נדחי ישראל יכנס׃
3 Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao.
הרפא לשבורי לב ומחבש לעצבותם׃
4 Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake.
מונה מספר לכוכבים לכלם שמות יקרא׃
5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.
גדול אדונינו ורב כח לתבונתו אין מספר׃
6 Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.
מעודד ענוים יהוה משפיל רשעים עדי ארץ׃
7 Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi.
ענו ליהוה בתודה זמרו לאלהינו בכנור׃
8 Yeye huzifunika anga kwa mawingu, huinyeshea ardhi mvua, na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.
המכסה שמים בעבים המכין לארץ מטר המצמיח הרים חציר׃
9 Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia.
נותן לבהמה לחמה לבני ערב אשר יקראו׃
10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.
לא בגבורת הסוס יחפץ לא בשוקי האיש ירצה׃
11 Bwana hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.
רוצה יהוה את יראיו את המיחלים לחסדו׃
12 Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni,
שבחי ירושלם את יהוה הללי אלהיך ציון׃
13 kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako.
כי חזק בריחי שעריך ברך בניך בקרבך׃
14 Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.
השם גבולך שלום חלב חטים ישביעך׃
15 Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi.
השלח אמרתו ארץ עד מהרה ירוץ דברו׃
16 Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu.
הנתן שלג כצמר כפור כאפר יפזר׃
17 Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?
משליך קרחו כפתים לפני קרתו מי יעמד׃
18 Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.
ישלח דברו וימסם ישב רוחו יזלו מים׃
19 Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.
מגיד דברו ליעקב חקיו ומשפטיו לישראל׃
20 Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake. Msifuni Bwana.
לא עשה כן לכל גוי ומשפטים בל ידעום הללו יה׃

< Zaburi 147 >