< Zaburi 145 >
1 Wimbo wa Sifa. Wa Daudi. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
Nitakutukuza wewe, Mungu wangu, Mfalme; nitalihimidi jina lako milele na milele.
2 Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
Kila siku nitakuhimidi; nitalisifu jina lako milele na milele.
3 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
Yahwe ndiye mkuu na wakusifiwa sana; ukuu wake hauchunguziki.
4 Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
Kizazi kimoja kitayasifu matendo yako kwa kizazi kijacho na kitatangaza matendo yako makuu.
5 Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
Nitaitafakari fahari ya utukufu wa adhama yako na matendo yako ajabu.
6 Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
Watanena juu ya nguvu ya kazi zako za kutisha, nami nitatangaza ukuu wako.
7 Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.
Nao watatangaza wingi wa wema wako, na wataimba kuhusu haki yako.
8 Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
Yahwe ni wa neema na huruma, si mwepesi wa hasira na mwingi katika uaminifu wa agano lake.
9 Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
Yahwe ni mwema kwa wote; huruma zake zi juu ya kazi zake zote.
10 Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.
Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe.
11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako,
Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako.
12 ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13 Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi.
14 Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
Yahwe huwategemeza wote waangukao na huwainua wote walioinama chini.
15 Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake.
Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi.
16 Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.
Huufungua mkono wako na hukidhi haja ya kila kiumbe hai.
17 Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo.
18 Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.
19 Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.
Hutimiza haja za wale wanao mheshimu yeye; husikia kilio chao na kuwaokoa.
20 Bwana huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza.
Yahwe huwalinda wale wampendao, lakini atawaangamiza waovu wote.
21 Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.
Kinywa changu kitazinena sifa za Yahwe; wanadamu wote na walitukuze jina lake takatifu milele na milele.