< Zaburi 140 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri,
למנצח מזמור לדוד ב חלצני יהוה מאדם רע מאיש חמסים תנצרני
2 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, na kuchochea vita siku zote.
אשר חשבו רעות בלב כל-יום יגורו מלחמות
3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao.
שננו לשונם כמו-נחש חמת עכשוב--תחת שפתימו סלה
4 Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu.
שמרני יהוה מידי רשע-- מאיש חמסים תנצרני אשר חשבו לדחות פעמי
5 Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, wametandaza kamba za wavu wao, wametega mitego kwenye njia yangu.
טמנו גאים פח לי-- וחבלים פרשו רשת ליד-מעגל מקשים שתו-לי סלה
6 Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.
אמרתי ליהוה אלי אתה האזינה יהוה קול תחנוני
7 Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita:
יהוה אדני עז ישועתי סכתה לראשי ביום נשק
8 Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu.
אל-תתן יהוה מאויי רשע זממו אל-תפק ירומו סלה
9 Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zinazosababishwa na midomo yao.
ראש מסבי-- עמל שפתימו יכסומו (יכסימו)
10 Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe.
ימיטו (ימוטו) עליהם גחלים באש יפלם במהמרות בל-יקומו
11 Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri.
איש לשון בל-יכון בארץ איש-חמס רע--יצודנו למדחפת
12 Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.
ידעת (ידעתי)--כי-יעשה יהוה דין עני משפט אבינים
13 Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako.
אך צדיקים יודו לשמך ישבו ישרים את-פניך

< Zaburi 140 >