< Zaburi 137 >
1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni.
Kando ya mito ya Babeli tuliketi na tulilia tulipokumbuka kuhusu Sayuni.
2 Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu,
Tulitundika vinubi vyetu kwenye miti ya Babylon.
3 kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”
Huko watekaji wetu walitaka tuwaimbie, na wale walio tudhihaki walitutaka sisi tufurahi, wakisema, “Tuimbieni moja ya nyimbo za Sayuni.”
4 Tutaimbaje nyimbo za Bwana, tukiwa nchi ya kigeni?
Tungewezaje kuimba wimbo unaomuhusu Yahwe katika nchi ya ugeni?
5 Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
Kama nikikusahau wewe, Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
6 Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa.
Ulimi wangu na ushikamane juu ya kinywa changu kama nisipokufikiria tena, na kama sipendelei zaidi Yerusalemu kuliko furaha yangu kuu.
7 Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, Bomoa mpaka kwenye misingi yake!”
Kumbuka, Ee Yahwe, kile walichofanya Waedomu siku ya anguko la Yerusalemu. Walisema, “Ibomoeni, ibomoeni mpaka chini kwenye misingi yake.”
8 Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, heri yeye atakayekulipiza wewe kwa yale uliyotutenda sisi:
Binti za Babeli, hivi karibuni wataharibiwa- mtu na abalikiwe, yeyote atakaye walipizia yale mliotufanyia sisi.
9 yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga na kuwaponda juu ya miamba.
Mtu na abarikiwe, yeyote achukuaye na kusambaratisha watoto wenu juu ya jiwe.