< Zaburi 137 >

1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni.
על נהרות בבל--שם ישבנו גם-בכינו בזכרנו את-ציון
2 Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu,
על-ערבים בתוכה-- תלינו כנרותינו
3 kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”
כי שם שאלונו שובינו דברי-שיר-- ותוללינו שמחה שירו לנו משיר ציון
4 Tutaimbaje nyimbo za Bwana, tukiwa nchi ya kigeni?
איך--נשיר את-שיר-יהוה על אדמת נכר
5 Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
אם-אשכחך ירושלם-- תשכח ימיני
6 Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa.
תדבק-לשוני לחכי-- אם-לא אזכרכי אם-לא אעלה את-ירושלם-- על ראש שמחתי
7 Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, Bomoa mpaka kwenye misingi yake!”
זכר יהוה לבני אדום-- את יום ירושלם האמרים ערו ערו-- עד היסוד בה
8 Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, heri yeye atakayekulipiza wewe kwa yale uliyotutenda sisi:
בת-בבל השדודה אשרי שישלם-לך-- את-גמולך שגמלת לנו
9 yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga na kuwaponda juu ya miamba.
אשרי שיאחז ונפץ את-עלליך-- אל-הסלע

< Zaburi 137 >