< Zaburi 134 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.
Njoni, mtukuzeni Yahwe, enyi nyote watumishi wa Yahwe, ninyi mnaotumika hekaluni mwa Yahwe wakati wa usiku.
2 Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana.
Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe.
3 Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.
Mungu na awabariki toka Sayuni, yeye aliye ziumba mbingu na nchi.

< Zaburi 134 >