< Zaburi 131 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.
Yahwe, moyo wangu haujivuni wala macho yangu hayana kuburi. Sina matarajio makubwa kwa ajili yangu mwenyewe wala kujihofia kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wangu.
2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.
Hakika nimejituliza na kuinyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa na mama yake, nafsi yangu ndani yangu iko kama mtoto aliye achishwa.
3 Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele.
Israeli, umtumainie Yahwe sasa na hata milele.

< Zaburi 131 >