< Zaburi 130 >
1 Wimbo wa kwenda juu. Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe.
2 Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.
Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma.
3 Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama?
4 Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.
Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa.
5 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.
Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia.
6 Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.
Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi.
7 Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.
Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe.
8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.
Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.