< Zaburi 13 >
1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini?
Mpaka lini, Yahweh, utaendelea kunisahau? Ni kwa muda gani utauficha uso wako nisiuone?
2 Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini?
Ni kwa muda gani nitalazimika kuhofu na kuhuzunika moyoni mwangu kila siku? Ni kwa muda gani adui zangu watanishida?
3 Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.
Unitazame na unijibu, Yahwe Mungu wangu! Nipe mwanga machoni pangu, vinginevyo nitalala katika mauti.
4 Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.
Usimuache adui yangu aseme, “Nimemshinda huyu,” ili kwamba asiweze kusema, “Nimemtawala adui yangu;” la sivyo, maadui zangu watafurahia nitakapo shushwa chini.
5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.
Lakini nimeamini katika uaminifu wa agano lako; moyo wangu wafurahia katika wokovu wako.
6 Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.
Nitamuimbia Yahwe kwa kuwa ameniganga kwa ukarimu kabisa.