< Zaburi 129 >
1 Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:
“Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme.
2 wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.
“Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda.
3 Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.
Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu.
4 Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.
Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.”
5 Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.
Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni.
6 Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;
Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua,
7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.
ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda.
8 Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”
Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”