< Zaburi 127 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure.
Yahwe asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure. Yahwe asipoulinda mji, aulindaye afanya kazi bure.
2 Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.
Ni kazi bure kwa wewe unayeamka mapema, na kulala kwa kuchelewa, au kula mkate kwa kuufanyia kazi ngumu, maana Yahwe huwapa chakula awapendao hata wawapo usingizini.
3 Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake.
Tazama, wana ni urithi kutoka kwa Yahwe, uzao wa tumbo ni thawabu kutoka kwake.
4 Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani.
5 Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.
Ni namna gani alivyo barikiwa mtu ambaye amelijaza podo lake hivyo. Hata aibishwa pindi atakapo kabiliana na adui zake katika lango.

< Zaburi 127 >