< Zaburi 123 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni.
Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.
2 Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia.
Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia.
3 Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi.
Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana.
4 Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.
Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.

< Zaburi 123 >