< Zaburi 122 >
1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.”
Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.”
2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.
Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako!
3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.
Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini!
4 Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli.
Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe.
5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.
Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! “Wote wakupendao wawe na amani.
7 Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.”
Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako.”
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, “Amani iwe ndani yenu.”
9 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.
Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.