< Zaburi 121 >
1 Wimbo wa kwenda juu. Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi?
Nitayainua macho yangu nitazame milimani. Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.
Msaada wangu unatoka kwa Yahwe, aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,
Hatauacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia.
4 hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.
Tazama, mlinzi wa Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi kamwe.
5 Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,
Yahwe ni mlinzi wako; Yahwe ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
Jua halitakudhuru wakati wa mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
7 Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako,
Yahwe atakulinda na madhara yote, na ataulinda uhai wako.
8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.
Yahwe atakulinda katika yote ufanyayo sasa na hata milele.