< Zaburi 118 >

1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
Give ye thanks unto Jehovah; for he is good; for his loving-kindness [endureth] for ever.
2 Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
Oh let Israel say, that his loving-kindness [endureth] for ever.
3 Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
Oh let the house of Aaron say, that his loving-kindness [endureth] for ever.
4 Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
Oh let them that fear Jehovah say, that his loving-kindness [endureth] for ever.
5 Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, naye akanijibu kwa kuniweka huru.
I called upon Jah in distress; Jah answered me [and set me] in a large place.
6 Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?
Jehovah is for me, I will not fear; what can man do unto me?
7 Bwana yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa.
Jehovah is for me among them that help me; and I shall see [my desire] upon them that hate me.
8 Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu.
It is better to trust in Jehovah than to put confidence in man;
9 Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu.
It is better to trust in Jehovah than to put confidence in nobles.
10 Mataifa yote yalinizunguka, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
All nations encompassed me; but in the name of Jehovah have I destroyed them.
11 Walinizunguka pande zote, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
They encompassed me, yea, encompassed me; but in the name of Jehovah have I destroyed them.
12 Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
They encompassed me like bees; they are quenched as the fire of thorns: for in the name of Jehovah have I destroyed them.
13 Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, lakini Bwana alinisaidia.
Thou hast thrust hard at me that I might fall; but Jehovah helped me.
14 Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu.
My strength and song is Jah, and he is become my salvation.
15 Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!
The voice of triumph and salvation is in the tents of the righteous: the right hand of Jehovah doeth valiantly;
16 Mkono wa kuume wa Bwana umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!”
The right hand of Jehovah is exalted, the right hand of Jehovah doeth valiantly.
17 Sitakufa, bali nitaishi, nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.
I shall not die, but live, and declare the works of Jah.
18 Bwana ameniadhibu vikali, lakini hakuniacha nife.
Jah hath chastened me sore; but he hath not given me over unto death.
19 Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru Bwana.
Open to me the gates of righteousness: I will enter into them; Jah will I praise.
20 Hili ni lango la Bwana ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.
This is the gate of Jehovah: the righteous shall enter therein.
21 Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu.
I will give thee thanks, for thou hast answered me, and art become my salvation.
22 Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni.
[The] stone which the builders rejected hath become the head of the corner:
23 Bwana ametenda hili, nalo ni la kushangaza machoni petu.
This is of Jehovah; it is wonderful in our eyes.
24 Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake.
This is the day that Jehovah hath made; we will rejoice and be glad in it.
25 Ee Bwana, tuokoe, Ee Bwana, utujalie mafanikio.
Oh save, Jehovah, I beseech thee; Jehovah, I beseech thee, oh send prosperity!
26 Heri yule ajaye kwa jina la Bwana. Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.
Blessed be he that cometh in the name of Jehovah. We have blessed you out of the house of Jehovah.
27 Bwana ndiye Mungu, naye ametuangazia nuru yake. Mkiwa na matawi mkononi, unganeni kwenye maandamano ya sikukuu hadi kwenye pembe za madhabahu.
Jehovah is God, and he hath given us light: bind the sacrifice with cords, — up to the horns of the altar.
28 Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.
Thou art my God, and I will give thee thanks; my God, I will exalt thee.
29 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
Give ye thanks unto Jehovah; for he is good; for his loving-kindness [endureth] for ever.

< Zaburi 118 >