< Zaburi 115 >

1 Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako.
לא לנו יהוה לא לנו כי לשמך תן כבוד על חסדך על אמתך׃
2 Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?”
למה יאמרו הגוים איה נא אלהיהם׃
3 Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo.
ואלהינו בשמים כל אשר חפץ עשה׃
4 Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
עצביהם כסף וזהב מעשה ידי אדם׃
5 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona;
פה להם ולא ידברו עינים להם ולא יראו׃
6 zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa;
אזנים להם ולא ישמעו אף להם ולא יריחון׃
7 zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
ידיהם ולא ימישון רגליהם ולא יהלכו לא יהגו בגרונם׃
8 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
כמוהם יהיו עשיהם כל אשר בטח בהם׃
9 Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.
ישראל בטח ביהוה עזרם ומגנם הוא׃
10 Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.
בית אהרן בטחו ביהוה עזרם ומגנם הוא׃
11 Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.
יראי יהוה בטחו ביהוה עזרם ומגנם הוא׃
12 Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni,
יהוה זכרנו יברך יברך את בית ישראל יברך את בית אהרן׃
13 atawabariki wale wanaomcha Bwana, wadogo kwa wakubwa.
יברך יראי יהוה הקטנים עם הגדלים׃
14 Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu.
יסף יהוה עליכם עליכם ועל בניכם׃
15 Mbarikiwe na Bwana Muumba wa mbingu na dunia.
ברוכים אתם ליהוה עשה שמים וארץ׃
16 Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, lakini dunia amempa mwanadamu.
השמים שמים ליהוה והארץ נתן לבני אדם׃
17 Sio wafu wanaomsifu Bwana, wale washukao mahali pa kimya,
לא המתים יהללו יה ולא כל ירדי דומה׃
18 bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana.
ואנחנו נברך יה מעתה ועד עולם הללו יה׃

< Zaburi 115 >