< Zaburi 113 >
1 Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana.
Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe.
2 Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele.
Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele.
3 Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa.
Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe.
4 Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu.
Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni.
5 Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,
Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu,
6 ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi?
atazamaye chini angani na duniani?
7 Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani,
8 huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
ili amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
9 Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana.
Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!