< Zaburi 112 >

1 Msifuni Bwana. Heri mtu yule amchaye Bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.
הללו יה אשרי איש ירא את יהוה במצותיו חפץ מאד׃
2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.
גבור בארץ יהיה זרעו דור ישרים יברך׃
3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele.
הון ועשר בביתו וצדקתו עמדת לעד׃
4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki.
זרח בחשך אור לישרים חנון ורחום וצדיק׃
5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki.
טוב איש חונן ומלוה יכלכל דבריו במשפט׃
6 Hakika hatatikisika kamwe, mtu mwenye haki atakumbukwa milele.
כי לעולם לא ימוט לזכר עולם יהיה צדיק׃
7 Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.
משמועה רעה לא יירא נכון לבו בטח ביהוה׃
8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.
סמוך לבו לא יירא עד אשר יראה בצריו׃
9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele; pembe yake itatukuzwa kwa heshima.
פזר נתן לאביונים צדקתו עמדת לעד קרנו תרום בכבוד׃
10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa, atasaga meno yake na kutoweka, kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.
רשע יראה וכעס שניו יחרק ונמס תאות רשעים תאבד׃

< Zaburi 112 >